Habari zenu wadau wahii blog?, Leo Nazungumzia kiufupi maisha ya muziki na wenyeji wa ifakara nikiwa kama prodyuza wa muziki na mwenyeji ifakara hii. kuna mambo ambayo nahisi ndio yanafanya musiki wa ifakara hauwezi kuendelea kabisaaaa, Cha kwanza kunatabia ya kupondani na kuchukia na baina ya wasanii hadi kuwaambukiza na maprodyuza wao ukitupia nje swala hilo kuna swala la kutopeana misaada sio wasanii hadi maprodyuza. hivi mwanzoni mwa mwaka huu 2013 nilikua safarini msumbiji na kwa muda wote studio yangu ilikua aifanyi kazi lakini kuna watu niliwaacha kama wakitaka kufanya kazi wafanye. Kilichotokea ni kuunda matabaka kati ya watu niliowaacha, kuna wanaonikubali na wengine hawanikubali na wamediliki hata kusambaza maneno kwa watu ili nionekane sina utu na nisithaminike huku watu hao hao ndio wananisubiri nikirudi wafanye kazi na mimi. Katika kufanikisha swala lao la usambaza maneno ambayo ayafai kunawatu yamewafikia na yamewagusa kwaiyo nilikuwa napigiwa sim nilipo na kuambiwa kila kinachoendelea. ila siku ya siku ilivyofikia kurudi nyumbani ifakara nilijifanya kama sijui chochote ili nifanye uchunguz wangu tangu nirud tarehe 29/03/2013 hadi hii leo 2/05/2013 nimefanikisha kuwajua masnichi wangu na wameamia studio nyingyine kwa aibu zao coz toka nijue nlikua siwafanyii kazi na nlibadilika nahis ndicho kiliwafanya wangundue kua nimejua na kuchukua jukum la kuhama huku nikisikia mapya kila siku katika midomo ya watu, wengine wanasema wanaanda nyimbo ya kunitukana wengine wanasema wanafanya njama zao ili nifeli katika kazi yangu sasa sijui wanataka kufanya nini. Ila hii tabia ya kijinga ya kuongeleana vibaya ipo saaaana huku ifakara sio kwenye musiki wala maisha ya kila siku. Kwaiyo kama weye ni mgeni wa huku kwetu basi jua kua haya mambo yapo na yapo saaaana. Ukiwa kama weye unaakili timamu unafikili sehemu kama hii ni ya kuishi na kufanya maisha ya ndio maisha yenyewe kama haya ya kusemana vibaya kila siku?. Hii ndio habari ya Ifakara na ndio maaana asilimia kubwa ya wanoendelea huku ni wageni.
Ahsante kwa kuielewa Ifakara kwa ufupi.
No comments:
Post a Comment