Ni katika Muundo mpya kabisa wa Studio mpya iitwayo dark city Music Ifakara Ambayo inafanya vizuri kwa sasa mjini ifakara na sehem mbalimbali za tanzania, kwa mahitaji ya burudani kwa wapenzi wa music na wadau wa Dark City Music Ifakara Producer Devil's touch na timu yake wameandaa show kwaajil ya wapenzi wa music pande za mbingu, Idete na sehemu nyingu tu za mkoa wa morogoro, ni katika kutambulisha studio na wasanii walio lebo katika studio yake. Ziara itaanzia Pande za Idete Siku ya jumamosi ya tarehe Ishirin na Saba ya mwez huu(27/04/2013) na kuendelea kwa maeneo mengine kwa siku tofauti na kwa taarifa ya matangazo na mipango ya wenyeji wa sehemu. kama weye ni mdau na show hii imeangukia pande zako basi usikose, hili ni bonge la show ambalo litaunganishwa na utafutaji wa waimbaji wasiojiweza kwa gharama za studio na kurekodiwa bure katika studio ya Dark City Music na kama kutakuwa na maelewano mazuri basi inaweza ikawa bahati ya kuwa lebo katika studio hiyo. Idete kaeni mkao wa kuwapokea Dark City Music Band Kwa burudani kabambe saaaaana.
No comments:
Post a Comment