Monday, August 27, 2012

Thabeet R. Shungu


Ass Director, Ass Camera Man, Ass Location Manager, Sound Manager wa I.T Video Production

Abdul Chalongite


Kamera Man, Story Writer, Location Manager, Derector & Video Producer wa I.T Video Production

Maandaliz Ya Video ya Mick Daddy




Mick Daddy Yupo katika maandaliz ya Shooting ya Nyimbo yake Iendayo kwa jina la Hip hop Kitengo cha juu chini ya mkono wa Forty Four(Ifoza Records) na Video Inasimamiwa na Kampuni ya I.T Video Production Ifakara Chini ya Camera Man Abdul Chalongite na Prod Faisal Jss na Kudailektiwa na B-Boi Stam na Abdul Chalongite, Hivi karibuni Itakuwa tayari kaeni mkao wa kula.

Maya

Maya Alifanya Vibaya Siku ya Eid Pili  Ndani ya Kumbi zilizopo Idete Akisindikizwa na Nukta Zero Dansaz, Maya Akiwaahid mashabiki wake wanyumbani hakisema sasa yupo chini ya Millionaire Republic Ikiongozwa na Sharo millionaire na hataharibu na msubiri kazi mpya na nzuri kuliko zilizopo hits hewani kwa sasa huku akisisitiza kuwa anamipango mingi sana na kampuni hiyo ya millionaire na kuahidi kuinyanyua Ifakara kwa ujumla.

Sherehe Za Eid Mosi Wilaya Ya Ulanga

Nukta Zero Dansaz Ndio waliokinukisha Vibaya Huko pande za Wilaya ya Ulanga Katika Kumbi nyingi tu katika kusheherekea Eid Mubbarack(Eid Mosi)

Friday, August 17, 2012

Hivi karibun nimepata tetesi ya kuwa msanii wa hip hop ndani ya mji mdogo wa Ifakara anayejulikana kwa jina la Man Shouk Ameenda kufanya ngoma mpya kabisa katika studio za Rocka Tz Records Morogoro town, Na nilipo wasiliana nae alinijuza kuwa ni kweli na itaachiwa baada ya kukamilika kutoka Studio na nilipohitaji mahojiano zaid alinambia kuwa atanitafuta akiwa na nyimbo mkononi ili tufanye mahojiano zaid kwahiyo kaa tayari kupokea nyimbo mpya kutoka kwa Man shouk

Friday, August 10, 2012

Show Kali Ndani ya Idd Mosi/Pili

Ni Fare Entertainment Inawaleta Bonge la show ya Uzinduzi wa Nyimbo na Video mpya Kabisa Kutoka kwa H.Fare Akisindikizwa na C-minor Kutoka Ifakara(Kwanza Label), Isa Malilo Kutoka Dar na Wakali wa Steji Ifakoda Nao watatumbuiza Vyakutosha. Siku ya Idd Mosi watafanya Show Katika Ukumbi wa Sanseti Chita na Idd Pili watafanya show katika ukumbi wa amani klabu. Mchana Kutakuwa na Disko toto kwa kiingilio cha shilingi Elfu moja(1000/=) na Usiku Mpaka majoo kwa Kiingilio cha Shilingi Elfu Mbili(2000/=) Usikose Mtu wangu.

Show Kali Ifakara(Idd Mosi)

Jamos Social Hall Inakuletea Show kali ya Wasanii nyota wa bongo fleva Siku ya Idd Mosi. Show Itaongozwa na Bright Ndaya Jamos social hall, Mchana kuanzia saa Sita Kutakuwa na disko toto kwa Kiingiko cha shilingi 1000/= Na usiku pia kuanzia saa mbili kwa kiingilio cha shilingi 2000/=. Show hii Imedhaminiwa na Big nation used center, Tonny Aluminium Glass na Tatu Bila bar. Show hii sio ya kukosa mtu wangu njoo tushuhudie mwanapakaya ametuletea vitu vipya kabisa

Sunday, August 5, 2012

Habar Nilizopata Hivi Punde

Ni Kwanza Records Ifakara yaanda Majeshi yake kwa Albam Moja moja kwa kila Mjeshi Ila bado aijatoa tamko kuwa lini zitakamilika Albam hizo. Kaa tayari kwa Kupata radha mpya kabisa kutoka kwa Man Luwanda Proffessor(Producer na Mmiliki wa Studio) Kwanza Records Ifakara.

Saturday, August 4, 2012

Kundi Jipya Ifakara!.

Karibu Ifakara Kwetu, Music na Sanaa za kutosha znapatikana na kumiminika kiila siku, Karibuni wageni woote, Leo sina cha kuwapa ila nina cha kuwadokeza kidogo kuhusu nini kinafanyika Ifakara Kwa sasa. Kuna kundi jipya kabisa Liitwalo Ifakara House Of Talent (I.H.T) ambalo lipo mbioni kufanya kazi zao yaani wanatarajia kushuti filamu zao kabambe na kali kabisa.Nyie kama wadau Subilieni mzigo mkali kutoka kwao.

I'm listening to in Hulkshare:

I'm listening to in Hulkshare: